KITU CHELSEA LEO KAZI NZITO UJERUMANI
0
Hatimaye Chelsea wanaingia uwanjani hii leo katika hatua ya mwisho ya jitihada zao za kutwaa Kombe la Mabingwa Ulaya.
Chini ya kocha wa muda, Roberto Di Matteo, Chelsea wana kazi ngumu bado, kwani watakuwa Allinz Arena, nyumbani kwa Bayern Munich, wakikabiliana nao kwenye fainali.Fainali ya wikendi hii ni wazi itakuwa ngumu kwa timu zote, huku Chelsea wakiwa wameshajijenga kisaikolojia na kujiamini kwamba wanaweza.
Hata kocha wa Bayern Munich, Jupp Heynckes anaamini kwamba, kwa timu yake kucheza nyumbani, ina nafasi kidogo tu juu ya Chelsea, anaosema ni hatari.
Ni mchezo unaosubiriwa na wengi, utakaokusanya mashabiki wengi katika uwanja wenye uwezo wa kubeba watu 66,000 katika mechi za kimataifa.
Chelsea wanaingia uwanjani wakijua ugumu wa mechi yenyewe, licha ya ukweli wa kuifunga Barcelona, kwa sababu Bayern Munich ni timu ngumu popote inapochezea, lakini pia itakuwa ikishangiliwa na maelfu ya mashabiki wake nikiwemo mimi mwenyewe.
