KUSHINDWA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI NI KUSHINDWA KAZI--Dk Shein

0
   Matatizo ya migogoro ya ardhi yaliyopo katika Wilaya ya Kusini Unguja,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein ,amewaweka katika kitanzi viongozi wa Mkoa wa kusini kwa kuwapa muda mfupi kutatua mgogoro uliopo bila hivyo atawawajibisha wahusika.
   Dk Shein alisema anatoa muda mfupi juu ya mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa kijiji cha kizimkazi kupatiwa jawabu lake na kama viongozi wa mkoa huo watashindwa tayari watakuwa wamempa jibu la kushinda kuwawajibikia wananchi wa mkoa huo.
   Alisema ataamua kuchukua hatua hiyo baada kuonyesha picha ndani ya taarifa ya mkoa huo kutomalizika suala hilo ingawa taafa hiyo kuelezea kuwa yamemalizika.
   Dk Shein aliyasema hayo wakati akifanya majumuisho ya ziara yake kwa mkoa wa Kusini Unguja,yaliyofanyika katika Chuo kikuu cha Zanzibar kilichopo Tunguu ,Wilaya ya kati Unguja.
   Dk Shein akiwa katika kijiji hicho kundi la vijana walijitokeza wakiwa na mabango yanayodai kutaka kuondolewa uongozi wa Wilaya hiyo kwa kile wanachodai kukerwa kwao kwa kuivunja kamati ya maendeleo ya kijiji.
   Baadhi ya mabango hayo yalidai kuitaka serikali ya Wilaya kunakosababishwa kutokukubaliana nayo kwa madai kutoipa uhuru kamati ya maendeleo ya kijiji hicho baada ya kuamua kutangaza kuivunja kutokana na kuiona inapingana na uamuzi wa Wilaya juu ya suala la viwanja.
    Akitoa maelezo ya ndani ya risala ya wananchi wa kijiji hicho mmoja wa wananchi hao ,mbele ya Dk Shein alisema wanasikitishwa sana kuona uongozi wa wilaya kuamua kuivunja kamati yao wakati tayari ishafanya kazi mbali mbali za maendeleo ya vijiji vinavyowazunguka eneo hilo.

0 maoni: