MIMI KUOLEWA JAMANI MMMH

0
Kiukweli  nimekuwa tofauti sana na wasichana wengi wa sasa hasa katika suaa zima la ndoa.Watu wengi sana wakiwemo baadhi ya ndugu kuniuliza kuhusu suala la ndoa,Maswali yamekuwa mengi sana na hata baadhi ya watu kuzungumza vile wanavyo weza.
   Unajua katika haya maisha kila mtu anautaratibu wake na malengo yake na siku zote kama unataka kufanikiwa naamini fanya kile unachoweza au unachohitaji kama unauwezo nacho,Mwanamke/Mwanaume siku zote unatakiwa ujiamini,uwe na msimamo na kile unachokifanya,ujikubali wewe mwenyewe,na unatakiwa ufanye maamuzi ambayo ni sahihi ili kusije kuwa na majuto baade,.
    Maisha kwa sasa yamebadilika kila kitu kiko juu,na hasa katika maisha ya ndoa ,Ingawa sijaingia ndani ya ndoa naamini ndoa inataka maandalizi makubwa sana,inatakiwa ujipange,na ukiamua kuingia ndani ya ndoa kuna vitu unatakiwa kuviacha kabisa na tayari unakuwa na majukumu kama mke/mume.
   Wasichana wengi wa sasa wanapenda kuiga kufuata mkumbo,fulani kaolewa basi ngoja na mimi nimlazimishe huyu boyfriend wangu anioe na mimi nionekane nimeolewa,jamani ndoa inataka makubaliano,kila mmoja amkubali mwenzie katika shida na raha,si kila mwanaume anaweza kuwa mume bora na wala si kila mwanamke anaweza kuwa mke bora,ndoa nyingi sasa hv hazidumu kwasababu watu wengi wanakurupuka,wanakimbilia ndani ya ndoa wakati bado mambo ya nje wanayataka.
  Mimi kuolewa mpaka nijipange,sitaki kuolewa kwa kufuata mkumbo kuwa fulani kafanya na mimi nifanye,muda ukifika naamini nitakuwa na maamuzi sahihi na naamini kile nitakachoamua kitakuwa sahihi hapo sasa  ndipo nitapanga na mume wangu tupate watoto wangapi naamini nitaishi kwa furaha zaidi kwasababu maamuzi yangu yatakuwa si ya kukurupuka,
    SITAKI KUOLEWA KWA AJILI YA KUNG'ARISHA NYOTA MJINI AU NA MIMI NIVAE PETE YA NDOA.NAAMINI SIKU ITAKAPOFIKA NITAFANYA MAAMUZI SAHIHI,
    INSHA'ALLAH  MALENGO NILIYOPANGA NA MCHUMBA WANGU NAAMINI MUDA UKIFIKA YATATIMIA KWA UWEZO WAKE MWENYEZI MUNGU NA BARAKA ZA WAZAZI PIA TUTAZIPATA,
   NIWAKUMBUSHE TU NA WALE WASICHANA WENZANGU AMBAO NA WAO WANAMPANGO WA KUKURUPUKA KUINGIA NDANI YA NDOA KWA KUIGA,JAMANI NDOA SI LELEMAMA MNATAKIWA MJIPANGE ILI TUPUNGUZE IDADI YA WAJANE NA TALAKA ZILIZOZAGAA KAMA NJUGU.

0 maoni: