JK AMWAGA MAWAZIRI 6,ATEUA WAPYA WATATU.

0

Rais Jakaya Kikwete amewapiga chini mawaziri sita kati ya nane waliotuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma.
  Akitangaza safu mpya ya mawaziri,Rais Kikwete amewaondoa aliyekuwa waziri wa Viwanda na Biashara Dk Cyril Chami,Waziri wa Fedha,Mustafa Mkulo,Waziri wa Afya Dk Haji Mponda,Waziri wa mawasiliano Ezekiel Maige,Waziri wa uchukuzi Omary Nundu na Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja.
    Naibu Mawaziri waliotemwa ni aliyekuwa Naibu Waziri  Afya Dk Lucy Nkya,na aliyekuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi Athuman Mfutakamba.
 Katika mabadiliko hayo Raisi Kikwete aliwateua mawaziri wapya watatu huku akiwapandisha naibu mawaziri wanne kuwa mawaziri,aliwateua manaibu waziri tisa,14 wamebaki katika nafasi zao za awali huku naibu mawaziri wawili wakitupwa nje.
    Rais Kikwete amewatangaza Steve Wasira kuwa waziri wa nchi ofisi ya Rais(uhusiano na Uratibu)George Mkuchika aliyekuwa waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI)George Mkuchika amekuwa waziri wa nchi ofisi ya Rais(Utawala Bora)na Celine Kombani amekuwa Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rasi(Utumishi)
   Ofisi ya Makamo wa Rais ameteuliwa Samia Suluhu kuwa Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) na Dk Terezya Huvisa kuwa Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Makamu wa Rais(Mazingira)

   Mawaziri waliopewa kuongoza Ofisi ya Waziri Mkuu ni Dk Mary Nagu,ambaye ameendelea kuongoza nafasi hiyo ya Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu(Uwekezaji na Uwezeshaji)Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi)Hawa Ghasia ambaye awali alikuwa Waziri wa nchi ofisi ya Rais(Utumishi)na William Lukuvi aliyebaki katika nafasi yake ya Waziri  wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge)

0 maoni: