MAWAZIRI WA EURO KUKUTANA LEO MJINI BRUSSELS

0
Mawaziri  wa  eneo  la  sarafu  ya  euro  wanakutana  leo huku  kukiwa  na  hali  ya  mtafaruku  kuhusu  Ugiriki pamoja  na  hali  ya  wasi  wasi  mkubwa  kuhusiana  na hali  ya  mabenki  nchini  Hispania  ikiwa  eneo  hilo  likifikia mwisho  wa  ufa  wa  mzozo  wa  madeni.


 Mawaziri  wa mataifa  17  wanachama  wa  umoja  wa  sarafu  ya  euro watakutana  mjini  Brussels  leo, kwa  lengo  la  kutoa ujumbe  mkali  kwa  vyama  vinavyohasimiana  nchini Ugiriki  kuwa  nchi  hiyo  inayokabiliwa  na  madeni inapaswa  kuheshimu  masharti  yaliyowekwa  mwezi March  kuhusiana  na  makubaliano  ya  mpango  wa uokozi  wa  uchumi. 
 Wataalamu  mbali  mbali  na  wadadisi pamoja  na  washirika  wa  kisiasa wa  umoja  wa  Ulaya wanaona njia nyingine ya  kulishughulikia  suala  la  Ugiriki ni  kwa  nchi  hiyo  kujitoa  katika  sarafu  ya  euro.  

0 maoni: